TIMU za Manispaa ya Ilemela zilizoingia Robo Fainali ya mashindano ya Angeline Jimbo, zimepatiwa vifaa vya michezo na mpira mmoja kwa kila timu.
Vifaa hivyo ambavyo ni jezi na soksii vimetolewa kwa timu zote nane leo na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kazungu Safari, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kazungu amekabidhi vifaa kwa timu za Nyakato, Kitangiri, Pasiansi, Ilemela, Shibula, Mecco, Bezi na Nyasaka na kuzipongeza kwa kufuzu hatua hiyo.
pharmacy
Ameahidi pia kwa timu zote zitakazofuzu hatua ya nusu fainali na fainali zitapewa tena jezi seti moja, soksi na mpira mmoja.
Naye mratibu wa mashindano hayo, Almas Moshi amesema michezo ya robo fainali itaanza Jumapili na kumalizika Jumatano.