Wapigaji fedha za miradi kukiona

ARUSHA; Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amekemea tabia ya wahandisi kuletewa fedha za miradi kutoka serikalini  na badala yake fedha hizo kuisha bila miradi kumalizika kisha kupanga kuongeza fedha  nyingine kutoka mapato ya ndani.

Mongella amesema hayo wilayani Longido baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya kata Mundarara na kupewa tarifa ya fedha zilizotolewa na serikali kiasi cha Sh,milioni 470 kuwa hazikukamilisha mradi huo na kupanga kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani.

Mbali na kuuagiza uongozi wa Wilaya ya Longido kukamilisha ujenzi wa mradi huo katika  maeneo yaliyosalia ifikapo Desemba 15, mradi ukuwa umezingatia vigezo vya ubora vilivyoainishwa na serikali, na kuwasisitiza kuhakikisha fedha zilizotolewa na serikali  zinakamilisha mradi huo bila kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani.

Advertisement

“Hii tabia ya kumaliza fedha za miradi halafu mnadai mtaongeza nyingine katika mapato ya ndani acheni,na kwanini Wilaya hii mnakuwa na miradi viporo au hammalizi miradi kwa wakati, jitahimini na mjipange katika usimamizi wa majukumu yenu, sitaki miradi viporo”

Rc ,Mongella alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marco Ng’umbi kuwasimamia watendaji wote wa chini yake, kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa fedha zilizoletwa na serikali.

Awali Serikali kupitia programu ya Kuboresha Miundombinu ya Shule za Sekondari Nchini (SEQUIP), imetoa Sh milioni 470 za kujenga shule mpya ya sekondari ya kata ya Mundarara, fedha hizo  zinazotumika kujenga vyumba 8 vya madarasa, jengo la utawala, majengo ya maabara, maktaba, chumba cha TEHAMA, matundu 16 ya vyoo pamoja na tanki kubwa la kuhifadhia maji .

9 comments

Comments are closed.