Wapigwa marufuku kuajiri watoto migodini

WAMILIKI migodi ya madini wilayani Mbogwe wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuajiri watoto wadogo kushiriki shughuli za migodini kwa kuwa watoto hao wanatakiwa kuwa shule.

Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea wachimbaji madini kwenye migodi iliyopo ndani ya wilaya hiyo akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya leo Oktoba 19, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed amesema kwa kutoajiriwa kwa watoto chini ya umri wa miaka 18 kutasaidia kudhibiti mdondoko wa elimu wilayani humo.

Amesema, ajira za watoto wadogo kwenye maeneo ya migodi yatahatarisha maisha yao na kuwanyima fursa ya kupata elimu ikiwa ni pamoja na kuwasababishia kutendewa matendo yasiyohakisi maadili ya Kitanzania ikiwemo kubakwa.

Advertisement

“Kumekuwa na tabia ya kuajiri watoto wadogo katika maeneo mengi ya migodi tambueni kuwa watoto hao wanakosa masomo na pia mnahatarisha afya zao, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakaye ajiri watoto katika mgodi wake’’.Amesema Sakina na kusisiitia

“Waacheni watoto waende shule, kama mnataka pambaneni na watu wazima wenzenu mchukue majukumu badala ya kuwadanganya watoto na kuwaachisha shule.”

Aidha, ametahadharisha kuhusu mmomonyoko wa maadili na kuwataka kuepuka kujihusisha na matendo yanayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

Pia amewatahadharisha wananchi kuhusu madhara ya mvua ambazo zimeanza kunyesha na kuwataka kuchukua hatua stahiki za kuepuka madhara yanayoweza kutokea ikiwa ni pamoja na kuanza kuondoka kwenye maeneo hatarishi ikiwemo maeneo ya mikondo ya maji.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *