Wapimwa homa ya ini bure Muhimbili

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili leo Julai 28, 2023 imetoa huduma ya vipimo vya ugonjwa wa homa ya ini  bure, ambapo matarajio ilikuwa kupima watu 500.

Akizungumza hospitali hapo ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani, Dk Eva Wiso wa Hospitali ya Muhimbili, ambaye ni  bingwa wa magonjwa ya mfumo wa chakula na magonjwa ya ini,  amesema takwimu zinaonesha  watu zaidi ya million 250 duniani kote wanaishi na virusi vya homa ya ini.

Advertisement

Amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kuongezewa damu isiyo salaa, vitu vyenye ncha kali na pia ngono isiyo salama.

Siku ya Homa ya Ini Duniani huadhimishwa Julai 28, ikiwa na lengo la kutoa elimu na hamasa kuhusu ugonjwa huo.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *