Wapinzani endeleeni na mikutano

DAR ES SALAAM: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda ameviasa vyama vya upinzani kuendelea na mikutano kwakuwa ndio afya ya siasa ya nchi na kipimo cha demokrasia ya kweli.

Akiwa katika mkutano na vyombo vya habari, Makonda asema raha yake ni kuona ushindani unakuwepo katika majukwaa ya siasa.

“Tunakula ruzuku za watu jamani, twendeni kwenye mikutano,” amesema Makonda wakati akiviasa vyama vya upinzani.

Makonda amesema kwake ushindani katika siasa ndio raha yake na ni sababu ya yeye kuwepo katika nafasi hiyo.

“Kutikisika kwa bahari, humpima nahodha shupavu.” Amesema Makonda.

Aidha, Katibu huyo ameviasa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuendelea kuhakikisha vyama vya siasa vinaendelea kutekeleza majukumu yake katika hali ya ushwari na usalama.

Una maoni usisite kutuandikia

Je umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness
#HabarileoUPDATES

Habari Zifananazo

Back to top button