Wapinzani wamshauri Zungu kusimamia maslahi ya nchi

WALIOKUWA wagombea urais wa vyama pinzani wamemshauri Spika mpya wa Bunge, Mussa Azzan Zungu aongoze mhimili huo wa dola kwa kuzingatia maslahi ya nchi pamoja na kuwaunganisha wabunge na si kuwagawanya.

Wagombea hao walitoa ushauri huo wakati wakizungumza na gazeti la HabariLEO.

Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), Mwajuma Milambo alimshauri Zungu kusimamia maslahi ya nchi, kusikiliza wabunge wote bila kujali vyama vyao, kuwaweka pamoja na si kuwagawanya kwa sababu wao ni sauti ya wananchi.

“Akasimamie uhuru wa hoja ya kila mbunge kwa sababu wabunge wote ni sauti ya wananchi, wapo pale kwa ajili ya kuwasemea wananchi, hivyo akaheshimu mawazo yao. Akasimamie malumbano ya hoja zenye tija na umoja wa kitaifa, ahakikishe kupitia uongozi wake bungeni Watanzania wanakuwa wamoja na anasimamia maslahi na misingi ya nchi,’’ alisema Milambo.

Aliongeza kuwa, Zungu anapaswa akumbuke wabunge wote wametumwa na wananchi na wana ahadi walizowaahidi, hivyo azibebe ahadi za kila mbunge ili kuchochea maendeleo ya wananchi na taifa kwa wakati.

Mwenyekiti wa Chama Cha Makini, Coaster Kibonde alimshauri Zungu kuhakikisha mhimili huo unafanya kazi yake sahihi ya kuisimamia serikali kutekeleza majukumu yake na si kuliongoza bunge kwa hisia.

“Namshauri asimamie bunge kwa weledi bila kujali itikadi zao za vyama. Awasimamie wabunge wote wawe
wachocheaji wa maendeleo ya wananchi na si maendeleo yao binafsi. Warudi kwenye majimbo yao wakahamasishe wananchi watunze amani, umoja na utulivu ili wakajenge Tanzania yenye uchumi imara
na wakatibu majeraha waliyoyapata baadhi ya wananchi kipindi cha uchaguzi,” alisema Kibonde.

Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru alisema Zungu ana uzoefu katika nafasi hiyo na anafahamiana na wabunge wengi, hivyo aepuke kufanya kazi kwa mazoea, bali akatimize majukumu yake kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi.

“Asitumie ubabe, aepuke dharau kwa mbunge yoyote na atumie busara, kwa sababu bunge linaongozwa na maadili, kanuni na sheria zake na ndio moyo na maono ya maisha ya Watanzania ulipo, kwa sababu pale ndipo maombi ya utatuzi wa kero kwa ajili ya maendeleo yao yanawasilishwa,” alisema Kunje.

Alimshauri kudhibiti utoro wa baadhi ya wabunge kwenye vikao vyote na majimboni kwao kwa kuwachukulia hatua ili kuongeza kasi ya maendeleo ya wananchi kwa maslahi ya taifa. Pia, ameshauri Naibu Spika wa Bunge kuteuliwa kutoka chama pinzani ili kuwa na usawa wa kidemokrasia.

Aliwashauri wabunge kufanya kazi kwa kutekeleza ahadi zao walizowaahidi wananchi wakati wakiomba kura, kutokana na viapo vyao na kwa kutenda haki ili wasilalamikiwe na wananchi.

Aliongeza: “Wasigeuze ubunge kama fursa au sehemu ya wao kujipatia maslahi yao binafsi, watumie uongozi wao kutatua kero za wananchi. Wananchi wengi wana maisha magumu, wakaangalie zaidi maslahi ya wananchi kwa sababu kupitia kura zao, wao ndio wamekuwa wabunge.’’

Alisema ni vyema wagombea hao wakatimize ahadi walizoziahidi ili watakaporudi tena kuomba kura, wananchi
wakawe na imani nao.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I was just looking for something flexible to do from home, and this turned out way better than I thought. It’s easy to start, doesn’t take much time, and it actually pays. Not one of those “too good to be true” things — just real work at home that fits your day.12

    Check it out → https://usbs0.blogspot.com/

  2. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  3. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button