Wapongezwa kutoa ardhi bila kudai fidia Bukoba

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imepanga kurudisha shukrani kwa wananchi wa Vijiji vya Itawa na Kangabusharo, Halmashauri ya Bukoba kwa kuzifanya shule zao za msingi na sekondari kuwa za mfano, baada ya kutoa ardhi bure ya kujenga tawi la Chuo Kikuu cha Dare es Salaam, bila kudai fidia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alifika katika ardhi hiyo, ili kukagua mahali kutakapojengwa chuo hicho na kuridhishwa na eneo lililotolewa na wanavijiji.

Amesema serikali itazifanya shule za vijiji hivyo kuwa za mfano, ambazo zitanufaika na programu mbalimbali za elimu.

Oktoba 13, mwaka huu wakati akizindua Chuo cha Ufundi Stadi Veta katika Kijiji cha Burugo, Rais Samia Suluhu Hassan, alimuagiza Waziri Mkenda kukagua ardhi ya ujenzi wa chuo kikuu mkoani Kagera.

Alisema ujenzi wa chuo hicho Mkoa wa Kagera unatarajia kuanza Machi 2023, endapo hati zote za ujenzi zitakuwa zimekamilika.

Habari Zifananazo

Back to top button