Wapongezwa mchango elimu kwa vijana

IDARA ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara imepongeza jitihada zinazofanywa na kikundi cha ujasiliamali (Navanji Enterprisses) kilichopo kwenye halmashauri hiyo kwa kutoa elimu hiyo kwa vijana.

Akizungumza wakati wa ghafla fupi ya utoaji vyeti kwa wahitimu wa mafunzo yaliyotolewa kwa wanafunzi wanne, Mkuu wa Idara hiyo Joyce Israel amesema kikundi hicho ni cha mfano hivyo kinapaswa kuigwa na vikundi vingine.

Wanafunzi hao ni wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Nangwanda kwenye halmashauri hiyo 2023.

Aidha bidhaa zinazotengezwa na kikundi hicho ikiwemo  za kemikali, kilimo, sabuni za maji na mche, mafuta, mkaa, biskuti, batiki, ubuyu, keki na zingine.

‘’Niwaombe msiishe hapa, muendelee kuibua na kuhamasisha wananchi hasa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu na wao kujiunga kwenye vikundi na kuwafundisha utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zitazowasaidia kupunguza umasikini na kukuza uchumi.’’amesema Israel

Mkurugenzi wa kikundi hicho, Ahme Naheka amesema kikundi chao kinatoa mafunzo kwa wajasiliamali na kutengeneza bidhaa hizo huku akiishukuru serikali kupitia halmashauri hiyo kwa kuwapatia msaada wa kitaalam, kiuchumi katika kuendesha shughuli zao.

‘’Wanafunzi waliyohitimu wamepata mafunzo ya miezi miwili na wapo tayari kufanya shughuli zao ambazo zitawaimarishia kipato chao cha kila siku na kuwaongezea uchumi hasa kwa mtu mmoja mmoja’’

Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Eslogiva George amesema mafunzo yamewasaidia kuwa katika mazingira salama na kupata maarifa yatakayowasaidia kuendesha maisha yao huku akitoa hamasa kwa vijana wengine kuchangamkia fursa hiyo kwani ni kama ilivyokuwa fursa nyingine.

‘’Hii ni fursa kama ilivyokuwa fursa nyingine na itatusaidia kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha zilizopo mtaani kwahiyo niwaombe sana vijana wenzangu kuwa fursa ndiyo hii wachangamkie’’

Habari Zifananazo

Back to top button