Warioba: Lowassa alikuwa na sifa za uongozi
DAR ES SALAAM; Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba amesema hayati Edward Lowassa ambaye alipata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, alikuwa na sifa za kibinadamu na za uongozi.
Warioba ametoa kauli hiyo leo Februari 13 wakati wa kuaga mwili wa Lowassa viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, shughuli iinayoendelea muda huu.
“Kwangu mimi Lowassa pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu, alikuwa ni kiongozi ambaye alikuwa na sifa za uongozi, ana imani kwamba anaweza kutumikia taifa, ana maono na ni mvumilivu,” amesema Warioba.
Lowassa alifariki dunia Jumamosi Februari 11, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam na anatarajia kuzikwa Februari 17 nyumbani kwake Monduli mkoani Arusha