Warudishwa gerezani kwa kukiuka mpango wa Parole

WAFUNGWA 29 wamekiuka masharti ya Mpango wa Parole na kurudishwa gerezani tokea Bodi ya Parole ilipoanza kusimamia utekelezaji wa sheria zake.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema hayo leo alipokuwa akizindua Bodi ya Taifa ya Parole.

Amesema wafungwa hao walikuwa miongoni mwa 5,678 ambao waliachiwa kwa mpango huo wa Parole.

“Serikali ilitunga sheria ya bodi za Parole ya mwaka 1994 na kanuni zake za mwaka 1997 ili kuhakikisha kwamba jamii ya watanzania inashirikishwa kikamilifu katika urekebishaji wa wahalifu,

“Kwa kuwapa wafungwa fursa ya kutumikia sehemu ya adhabu zao wakiwa nje ya magereza kwa usimamizi wa jamii nzima,” amesema.

Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mzee Ramadhani Nyamka amesema tangu bodi hiyo ianze kusimamia utekelezaji wa sheria ya Bodi za Parole, h iyo ni awamu ya nane ya vipindi vya miaka mitatu mitatu ya utendaji wake.

Na kwamba mpaka sasa vikao 46 vimeshafanyika tangu ianzishwe sheria hizo.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button