Wasafiri Katavi wapongeza utaratibu wa sensa

BAADHI ya wananchi waliokuwa wakisafiri kuelekea maeneo mbalimbali nchini kutokea mkoani Katavi, wameipongeza serikali kwa namna ilivyoratibu sensa mwaka huu.

Wakizungumza baada ya kuhesabiwa katika stendi kuu ya mabasi ya Mizengo Pinda, wamesema sensa ya mwaka huu imekuwa na hamasa kubwa na hata zoezi lenyewe linaendeshwa kisasa.

“Binafsi nimehesabiwa hapa stendi na nimefurahi zoezi lilivyoenda, niwashauri tu wale, ambao bado hawajafikiwa wasiwe na hofu, kwani zoezi hili linaendeshwa kisasa na kingine niwaombe kutoficha taarifa,”alisema Specioza Daniel.

Katika hatua nyingine walinzi wa klabu za usiku mjini Mpanda, wamewazuia makumi ya wateja wao kuingia kwenye klabu hizo isipokuwa wale waliokuwa na vitambulisho maalumu vilivyotolewa kwa watu waliohesabiwa.

Kwa upande wake mratibu wa Sensa Manispaa ya Mpanda, Paul Kahoya, ambaye aliambatana na makarani usiku, amesema zoezi limeenda kama lilivyopangwa na kuongeza kuwa ni imani yake kuwa litakamilika kwa utaratibu uliowekwa.

Habari Zifananazo

Back to top button