WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu, ameiasa jamii kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watu wenyechangamoto ya afya ya akili, badala yake wawasaidie kupata matibabu.
Waziri Ummy aliyasema hayo katika mdahalo wa afya ya akili, uliofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
Amesema kumekuwa na tabia ya watu kuwaita wagonjwa wenye changamoto ya afya ya akili kuwa ni chizi na vichaa, hali inayowaondolea uwezo wa kujiamini.
“Kila mtu anaweza akapata changamoto ya afya ya akili, lakini atalikabili vipi akienda hospitali anaa biwa chizi, kichaa, hawajui kupata tatizo la afya ya akili ni kitu cha kawaida, kama vile tunapata homa, tunaumwa kichwa kwa hiyo hata afya ya akili huwezi kukwepa kupata,” ameeleza.