Wasakwa tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi
JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro kupitia Dawati la Jinsia na Watoto linawasaka wanaume wawili waliotoweka baada ya kutuhumiwa kuwapa mimba wanafunzi wawili wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 15 na mwenzake wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 17.
Wanafunzi hao wote ni familia moja ya Simon Zongo na mkewe Neema Kenge (39) wenye watoto 13 kati ya waliowazaa 15 na mkazi wa Mtaa wa Mgonahazeru ,Kata ya Mbuyuni, Manispaa ya Morogoro na kusababisha kukatisha ndoto zao za msomo .
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ,Pendo Meshurie amesema hayo Februari 2, 2024 wakati alipoitembelea familia hiyo.
Meshurie amesema Dawati la Jinsia na Watoto la jeshi hilo ngazi ya wilaya liliibua suala hilo kupitia kwa mratibu Polisi kata ya Mbuyuni ambaye alifikisha kwenye dawati kuieleza mkasa ulioipata familia hiyo na kuanza kulifanyia kazi.
Amesema walifika katika familia hiyo na kukutana na mke wa mume huyo Neema mwenye watoto 15 aliowazaa wakiwemo hao wawili ambao wamepata ujauzito ili kupata taarifa za kina zaidi.
“ Nituweza kuzungumza na Neema na amekiri ni kweli ana watoto 15 , ameolewa na ana mume wake wanaishi pamoja na wanaishi kwenye nyumba ya vyumba viwili kimoja cha wazazi na kingine ni cha watoto …anafamilia kubwa lakini ni nyumba ni ndogo” anasema Meshurie
Meshurie amesema walibaini kuwa wapo watoto wakike ambao wameshindwa kutimiza ndogo zao za kimasomo kwa kupata mimba wakiwa ni wanafunzi mmoja ni wa kidato cha kwanza ( jina lake limehifadhiwa ) na mwingine darasa la saba ( pia jina lake limehifadhiwa ).
Wanafunzi hao waliopata mimba mmoja wao wa darasa la saba yeye anatarajia kujifungua wakati wowote kuanzia sasa ambao wote wanamtengemea mama yao kwa kila jambo licha naye ana mtoto mchanga wakike .
“ Tuliongea na kumuuliza kwanini hakufika kituo cha Polisi kutoa taarifa ya watoto wake hao ambao ni wanafunzi kupewa ujauzito huo mapema …na alichokijibu ya kwwamba hakuona umuhimu wa kufika kituo cha Polisi kutoa taarifa hiyo “ amesema Meshurie.
Amesema pia waliwahoji watoto hao wakike ambao ni wanafunzi , wao walikiri ya kwamba wamepewa mimba lakini na watu ambao wamekimbia ,hawajui wanaume waliowapa ujauzito huo kwa sasa wako wapi .
Meshurie amesema kutokana na wanaume hao kutoweka walieleza hawakuona umuhimu wa kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi.
“ Sisi Dawati baada ya kufika kwenye familia hii tumebaini hilo na tulichukua hatua na tumeaanza upelelezxi wetu na hatua zetu za kisheria tunaendelea kuzifanya na tunaamini tutafika tunako taka ili kuisaidia familia hii “ amesema Meshurie.
Meshurie amesema kuwa jitihada za kuwatafuta wanaunme hao waliowapa mimba wanafunzi zinaendelea na taratibu zitakapokamilishwa litafikishwa shauri hilo kwenye mamlaka zianzohusika ili taaratibu ziweze kuchukuliwa .
Alisema kwa sasa wanafanya jitihada za kumpa mume wake ili afike ofisi za dawati ili kupata maelezo mengi zaidi kutoka kwake kwani hadi sasa bado hawajakutana naye ana kwa ana kutoka na shughuli zake za ulinzi wa usiku .
“ Kwa kuwa suala hilo tumelipata muda mfupi , tumempa muda mume wake afike Kituo cha Polisi dawati la Jinsia na watoto ili kuongea nane kwa vizuri zaidi” amesema Meshurie.