Wasanii kibao waula filamu ya Toboa Tobo

DAR ES SALAAM; WATANZANIA zaidi ya 60 wamepata nafasi ya kazi katika tamthilia ya Toboa Tobo inayoongozwa na mzalishaji na muandaaji wa filamu, Devotha Mayunga.

Akizungumza na HabariLEO, Devotha amesema idadi hiyo inajumuisha waigizaji 44 na watu wa operesheni tofauti 18 ambao wanakamilisha filamu hiyo.

“Hadi sasa hivi mimi mwenyewe narudisha vitu kwa jamii maana nina watu zaidi ya 50 nimewaajiri kupitia series yangu ya Toboa Tobo,” amesema Devotha.

Pia amezungumzia soko la nje ambapo amesema kwa sasa changamoto yake ni ushindani tu.

Amesema katika suala la vifaa na watalamu hakuna shida kwani wanao na vifaa pia vipo.

Habari Zifananazo

Back to top button