Wasanii kujiheshimu ndio kila kitu

DAR ES SALAAM: Wasanii nchini wametakiwa kujiheshimu ili kulinda na kutunza utu na majina yao kwa vizazi vyao vya sasa na baadae katika jamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bejez Company maarufu kama Mwamba wa Bahari, Shabani Mwanga, wakati akitambulisha wasanii wa Filamu nchini kama mabalozi wa Kampuni hiyo.

“Nilivyokuwa nafikiria wasanii wa  kuwapa ubalozi niliwaza msanii awe na heshima na hekima katika jamii sio wa kuchafua hali ya hewa muda wowote.”

Advertisement

Amesema  wasanii waliopata bahati ya kuwa mabalozi wa kamapuni hiyo ni Rihama Ally Mwogomchungu, Niva Kulwa Kikumba, ‘Dude’ pamoja na Tine White na kigezo kilichowabeba ni heshima waliyonayo katika jamii.

“Kuna wasanii wana majina kiasi kwamba akiwa balozi wa kitu fulani kitafahamika kwa haraka lakini hawajiheshimu hawana maadili mazuri kwenye jamii.”

“Hata uwe na pesa kiasi gani kama huna maadili watu hawana cha kujifunza kutoka kwako huna chakufundisha watu kwenye jamii.”amesema Shabani

Pia ameongeza kuwa “watakuwa mabalozi wazuri watakaotangaza mwamba wa Bahari wanaokuletea mzigo kwa bei unayotaka wewe.”

1 comments

Comments are closed.