“Wasanii lindeni haki za watoto”
DAR ES SALAAM: Wasanii wametakiwa kulinda watoto wanapokuwa wanafanya kazi zao za Sanaa kwa kufuata utaratibu na haki za mtoto kwa kuangalia muda na shughuli wanazo wapa watoto.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa BASATA Dk Kedmon Mapana amesema kuwa watoto wanahaki zao nasio kuwafanyisha kazi za kunengua.
“Watoto hawapaswi kufanyakazi yoyote usiku muda wa kulala hata kama anakipaji anatakiwa awe nyumbani awe amepumzika nasio wasanii kuwageuza watoto kuwa madansa jambo ambalo sio zuri.
“Kuna sheria inayomlinda mtoto kutofanyakazi na kujihusisha na shughuli zozote za usiku katika ukumbi na uwanja wa wazi.
” amesema Dk Mapana.