Washauri kuzingatia mwongozo wa manunuzi

WATAALAM kutoka idara mbalimbali mkoani Mtwara wametakiwa kuzingatia mwongozo wa manunuzi wanaopatiwa sasa ili kuongeza tija katika eneo la manunuzi ya umma.

Hayo yameelezwa wiki hii katika mafunzo ya siku tano yanayoendelea mkoani humo kwa wataalam hao kuhusu kuwajengea uwezo ili waweze kuelewa matumizi sahihi ya mfumo mpya wa manunuzi (NeST) uliyozunduliwa rasmi Julai 1, mwaka huu.

Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Manunuzi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Theresia Nsanzugwanko alisema ujio wa mafunzo hayo utasaidia kupunguza baadhi ya malalamiko mbalimbali ya ucheleweshwaji huduma katika idara hiyo ambao kwa namna moja ama nyingine haukuonyesha mafanikio mkubwa kama matarajio ya serikali yalivyokuwa.

Advertisement

Aidha, serikali imaenzisha mfumo huo ili kuhakikisha thamani ya fedha inayotumika katika manunuzi ya aina yoyote inaendana na kiwango cha ubora wa huduma zinazotolewa hivyo baada ya kuona mfumo uliyokuwa ukutumika awali wa TANePS haukidhi malengo ya manunuzi ya umma.

Miongoni ni ucheleweshaji utoaji huduma imeamua kuanzisha mfumo huo mpya wa NeST ambao utakuwa mwarobaini wa kufuta changomoto zote kwenye mfumo wa awali.

‘’Hii NeST sasa imekuja kama mwarobaini ya kufuta yale yote ambayo yalikuwa na changomoto kwenye mfumo wa awali wa TANePS ambao haukukidhi malengo ya manunuzi ya umma ikiwemo kuruhusu mianya iliyokuwa ikichelewesha utoaji wa huduma  kwahiyo haya maboresho sasa kwa kiasi kikubwa yataongeza ufanisi katika eneo hilo’’, Nsanzugwanko

Ofisa manunuzi kutoka halmashauri ya mji Nanyamba, Yusufu Mrisho alisema mfumo huo utaenda kurahisisha utendaji katika idara hiyo pamoja na zingine kwasababau unaenda kuwa wazi kwenye utekelezaji wa majukumu yao hayo kwa kuwa mtu ananaweza kuingia moja kwa moja katika mfumo husika kuona namna ambavyo kazi ya manunuzi imefanyika.

Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu manisapaa ya mtwara mikindani, Gwakisa John alisema kwa sasa watajaza manunuzi kwa kutumia mfumo tofauti na hapo awali walikuwa wakifanya manunuzi bila utaratibu hivyo utaratibu huo utarahisisha upatikanaji wa vitu kwa haraka.

1 comments

Comments are closed.