Washitakiwa 2 uhujumu uchumi wapata dhamana

WAKAZI wawili wa Dar es Salaam, Jayzan Kuchar maarufu kama China na Aloyce Francis wanaokabiliwa na mashitaka matatu ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na vipande 19 vya meno ya tembo, wamepewa dhamana baada ya kutimiza masharti.

Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio alisema hayo juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mshitakiwa kuwasilisha masharti ya dhamana ya kugawana dhamana ya hati ya mali yenye thamani ya Sh milioni 70.

Mrio alisema moja ya masharti ya dhamana ni kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 35 kwa kila mshitakiwa.

Advertisement

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 25, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa tena.

Awali, Wakili wa Serikali, Caroline Matemu alidai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya uamuzi wa dhamana na washitakiwa wote waliieleza mahakama kuwa wako tayari.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *