Wasichana 1000 Mwanza kufundishwa ujasiriamali

ZAIDI ya wasichana 1000 kutoka Wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Imarisha Wasichana.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Sauti ya Wanawake Ukerewe, Sophia Donald, wakati mahojiano malumu na HabariLeo.

‘’Mradi wa Imarisha Wasichana ulianza Oktoba 1 na unatarajia kukamilika Septemba 2023. Katika wilaya ya Ilemela wanaufaika watatoka kata za Nyakato, Kahama, Buswelu, Ibungilo, Kiseke na Nyasaka,’’ amesema Donald.

Amesema kupitia mradi huo, wasichana watajifunza kuhusu ujasiriamali pamoja na kufundishwa kuhusu haki zao, ili waweze kujitambua kiuchumi.

Amesema kupitia mradi huo wasichana watafundishwa mafunzo ya kutengeneza urembo pamoja na ushonaji nguo, ambapo wanufaika watajiajiri kupitia vikundi na kuongeza kuwa pia watajifunza kuhusu afya ya uzazi salama.

Mkazi wa Ilemela Shamira Valentine amesema amefanikiwa kujifunza ujasiriamali wa kushona nguo, kutengeza maua na sabuni za maji.

 

Habari Zifananazo

Back to top button