Wasichana Geita, Kigoma wapatiwa baiskeli

SHIRIKA la Plan International, limejitolea baiskeli 500 kwa wanafunzi wa kike wanaoishi katika mazingira magumu, ili kuwaondolea adha ya usafiri waendapo shule na kuwapunguzia hatari ya vitendo vya ukatili wa kingono.

Msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwezesha Mabinti Balehe Kuendelea na Masomo (KAGIS), unaosimamiwa na shirika hilo katika mikoa ya Geita na Kigoma chini ya ufadhili wa Watu wa Canada (CAG).

Akizungumuza wakati wa hafla ya utoaji baiskeli hizo mjini Geita, Mkurugenzi wa Miradi Plan International Tanzania, Peter Mwakabwale, amesema baiskeli 300 zimetolewa kwa wasichana wa Mkoa wa Geita na 200 mkoani Kigoma.

Amesema hiyo ni awamu ya kwanza ya mpango huo na hadi kukamilika kwa mradi wa KAGIS wamepanga kununua na kugawa jumla ya baiskeli 2,000 kusaidia kufikiwa azma ya upatikanaji sawa wa elimu msingi kwa makundi yote.

“Tumetambua changamoto ya kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni hasa kwa shule za sekondari, inasababisha wasichana hawa kukabiliana na vishawishi vinvyopelekea kukatisha masomo,” ameeleza.

Akizungumuza kwa niaba ya wanufaika, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Bung’wangoko, Aneth Jospeh amekiri msaada utawasaidia kuhudhuria masomo kila siku na kuepukana na hatari ya kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kata Ihanamilo, Salum Mkumala, amesema mradi utahamasisha mahudhurio ya wanafunzi ikiwemo wasichana ambao wanatembea si chini ya umbali wa Kilometa 90 kwa siku kufuata masomo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x