‘Wasichana jifunzeni fani ya vipuri’

WASICHANA wamehimizwa kujifunza zaidi fani ya vipuri, ili waweze kujiajiri kwani fani hiyo inamuwezesha mkufunzi kupata soko la ajira.

Akitoa rai hiyo Mkufunzi kutoka Chuo cha Ufundi Stadi Veta Moshi, Baraka Lauo kwenye Maonesho ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) jijini Arusha.

Advertisement

Amesema katika chuo cha Veta Moshi, mkoani Kilimanjaro wanafundisha kozi za aina mbalimbali ikiwemo hiyo ya utengenezaji wa vipuri vya aina mbalimbali zinazohitajika katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Veta-Moshi tunatoa kozi ya utengenezaji vipuri na soko lipo, lakini mwamko wa watoto wa kike ni mdogo katika kozi hii, hivyo nawahimiza wasichana wajiunge katika kozi hii inayojiuza yenyewe,” amesema.

 

/* */