Wasiojisajili waondolewe – Rais Samia

RAIS Samia Suluhu  amewataka mawakili wa Serikali ambao hawajajisajili kwenye daftari la mawakili wa Serikali wafanye hivyo  kabla muda haujamalizika.

Rais Samia amesema hayo leo Alhamisi ya Septemba 29, 2022 akifungua mkutano wa kuanzishwa chama cha kitaaluma cha mawakili wa Serikali jijini Dodoma.

Amesema mawakili  ambao bado hawajajisajili, wahimizwe  wajisajili, vinginevyo baada ya muda kupita hawatatambulika kama ni mawakili wa serikali

“Muda ukipita Itabidi tu tuwaondoe ama watafute sekta nje waingie, ama sijui watapewa msamaha gani na Mwanasheria Mkuu ili waingie tena kama mawakili wa Serikali.

“Amri ikitoka mnapaswa kutekeleza, labda mtu awe na dharura ya muhimu sana labda mgonjwa hospitali. Mwanasheria Mkuu simamia hilo.

Rais Samia amesema taarifa alizonazo ni kuwa hadi  sasa mawakili wa Serikali ni 2,652 na kuna wengine bado hawajajisajili kwenye daftarri hilo ambalo liko kwa mujibu wa sheria.

Kauli ya Rais Samia imekuaj wakati Wizara ya Katiba na Sheria kuanzisha kanzi data ya wanasheria walio katika utumishi wa umma ili kuiwezesha Wizara kuwafahamu, kujua taaluma zao, uzoefu wao, ubobefu wao na wapi walipo ili kuiwezesha Serikali kutumia uzoefu wao kuleta matokeo chanya nchini na kuwaondoa vishoka wa sheria.

Habari Zifananazo

Back to top button