Wasiojulikana waiba kichanga Bukoba

WATU wasiojulikana wameiba mtoto wa mwezi mmoja aliyefahamika kwa jina la Benitha Benedict ambaye wazazi wake ni wakazi wa Migera Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Hakuna sababu iliyotolewa yakupelekea kichanga hicho kuibwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera William Mwampaghale amesema tukio hilo limetokea Disemba Mosi mwaka huu majira ya 6:00mchana Nyumbani kwa mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Johanitha Agustina.

Mwampaghele amesema Johanitha aliliambia Jeshi la Polisi kuwa akiwa Nyumbani anaendelea na shughuli zake mwanae alikuwa amelala chumbani alipokea wageni watatu waliokuja kumpongeza na baada ya mazungumzo aliwasindikiza akimuacha mtoto nyumbani.

“Wakati akiwasindikiza walitokea watu wawili waliotaka kuzungumza naye hata hivyo alikataa akidai anawasindikiza jamaa waliokuja kumpongeza na aliporejea nyumbani hakumkuta mtoto,” Mwampaghele amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button