Wasiorejesha mikopo kuchukuliwa hatua

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imevitaka vikundi vyote vya Manispaa ya Morogoro ambavyo havijafanya marejesho ya mikopo zaidi ya Sh milioni 600 kuhakikisha vinarejesha mapema iwezekanavyo kabla havijachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa Takukuru mkoa huo ,Manyama Tungaraza alitoa kauli hiyo Agosti 11, 2023 mjini Morogoro kwenye taarifa yake kwa umma kuhusu utendaji kazi zilizofanyika katika kipindi cha Aprili 2023 hadi Juni 2023 .

Tungaraza alisema katika kipindi hicho Takukuru ilifanya uchambuzi wa mifumo ya mianya ya rushwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya usimamizi wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi maalumu ya wanawake , vijana na wenye ulemavu .

Alisema kilichobainika kutokana na uchambuzi huo kwa Manispaa ya Morogoro ni kwa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kutolewa bila kufuata utaratibu, mikopo kutorejeshwa kwa wakati na kutolewa tofauti na malengo ya kikundi .

Tungaraza alisema hatua zilizochukuliwa kwa Manispaa ya Morogoro, ni Takukuru kusimamia urejeshwaji wa fedha za mikopo kwa vikundi ambavyo havijakamilisha madeni yao .

“ Kwa Manispaa ya Morogoro ina zaidi ya Sh milioni 600 ambazo hazijarejeshwa tangu mwaka jana na tumewaomba karibu kata zote 29 isipo kuwa vikundi vichache vimerejesha,”

“…hizi fedha zingetumika kwa kazi nyingine lakini Watanzania wa manispaa wamekopeshwa na walipaswa kutekeleza jinsi mikipo inaavyoelekeza. “ alisema Tungaraza

Alisema zipo taarifa ya kwamba sehemu kubwa ya vikundi vilivyokopeshwa kupitia mpango huo vimeshindwa kufanya marejesho kwa wakati kitu ambacho kinakwamisha vikundi vingine kuendelea kupata mikopo hiyo.

“ lakini waliokopeswa wamezitumia fedha hizo kwa matumizi tofauti na kushindwa kurejesha kwa wakati ili mikopo hiyo iendelee kuwanufaisha wengine.” alisema Tungaraza.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button