Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa, amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwalea watoto katika misingi ya dini, Ili kutengeneza kizazi chenye hofu ya Mungu.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga mashindano ya kuhifadhi Quran tukufu yaliyohusisha shule zote za taasisi ya Ansaar zilizopo nchini Tanzania.
Amesema kuwa ukiwaanda watoto katika misingi ya kumjua Mungu na kuhifadhia Quran tukufu wataweza kuwa watu wema wakiwa wakubwa na wenye hofu ya Mungu.
“Niwaombe wazazi Ili tuweze kuwa na kizazi chenye hofu ya Mungu, lazima tuwabidiishe katika kusoma elimu ya dini bila kusahau elimu ya dunia, Ili waweze kuwa raia wema hapo siku za mbeleni,”amesema DC Mgandilwa.
Naye Mudir wa taasisi hiyo, Salim Barahian amesema kuwa shule zilizopo katika taasisi yake licha ya kufundisha elimu ya kawaida, poa elimu ya dini wamekuwa wakiitilia mkazo.
“Licha ya kufuata miongozo ya utoaji wa elimu inayoendana na misingi ya serikali, lakini elimu ya dini nayo tunaipa kipaumbele oli kuwa na vijana nora wanaomtambua Mungu na kufuata maamrisho na misingi ya dini inavyoelekeza,”amesema Barahian.