“Wastani wa umri wa kuishi Watanzania ni miaka 65”

Wanawake wanaishi umri mkubwa zaidi

DAR ES SALAAM: Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk Albina Chuwa amesema Juhudi za Serikali katika kuendelea kuimarisha sekta ya afya zimezaaa matunda ambayo ni kuongeza wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania.
Dk Chuwa amesema miaka ya nyuma wastani wa kuishi wa Watanzania ilikuwa ni miaka michache akisema mwaka 1978 wastani wa umri wa kuishi wa Watanzania ulikuwa ni miaka 44 lakini kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 takwimu zinaonesha kuwa wastani huo umeongezeka na kufikia asilimia 65.5.
Amesema katika takwimu hizo wanawake ndio walio na wastani mkubwa zaidi ambapo wastani wao wa kuishi ni miaka 69 huku wanaume wakiwa na wastani wa kuishi miaka 62 kutokana na sababu mbalimbali katika jamii.
Dk Chuwa ameyasema hayo Oktoba 28, 2023 katika Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam na kuongeza
 
Malengo ya Ripoti ya utafiti huo ni kujua maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma za afya ili kuyafanyia kazi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
1 month ago

Work At Home For USA My buddy’s aunt makes $64/hr on the computer. She has been unemployed for eight months(ga) but last month her but pay check was $12716 just working on the computer for a few hours.
Check The Details HERE……… http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x