Wataalam 16 wa Marekani kujitolea nchini

WAFANYAKAZI 16 wakujitolea Raia wa Marekani wameapishwa mbele ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle sambamba na muwakilishi wa mgeni rasmi Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dk Edith Lwiza kwaajili ya kuhudumu katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya na elimu.

Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam katika makao Makuu ya Peace Corps nchini ikiwa ni mara ya kwanza kuhudumu tangu kutokea kwa janga lililoukumba ulimwengu UVIKO 19 mwanzoni mwa Machi 2020.

Wakitoa hotuba yao wataalamu hao wamezungumzia namna walivyonufaika na wiki 11 za mafunzo katika chuo cha mfunzo wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga.

“Kesho tutapanda boti, mabasi na kwenda mbali na sehemu tulizozizoea kwaajili ya kutekeleza yale tuliyojifunza.”

Mkurugenzi wa mafunzo wa Peace Corps, Fortunata Mufundi amesema vijana hao wamejifunza tamaduni za kitanzania ikiwemo Lugha ya Kiswahili, vyakula, historia na mifumo ya maisha ya kila siku kwa watanzania wa mijini na vijijini

“Vijana hawa wametoka katika majimbo 11 nchini Marekani ikiwemo Chicaco, California, Massachusetts hivyo tunataraji vijana hawa wawe mabalozi wazuri wa nchi ya Tanzania.”

Akizunguka kwa niaba ya Waziri Kairuki, Dkt. Edith Lwiza amewaasa vijana hao licha ya upweke watakaokuwa nao wanapoelekea kutengena katika kuhudumu maeneo tofauti nchini wanapaswa kuzingatia yote waliyojifunza walipokuwa mafunzoni Korogwe

Itakumbukwa, Peace Corps ilianzishwa nchini Marekani mwaka 1961 na Rais wa wakati huo Hayati John F. Kennedy na tayari imeshahudumu katika nchi 142 duniani ikiwa Tanzania imeshapokea wafanyakazi 3200 tangu kuanzishwa kwake hadi sasa

Habari Zifananazo

Back to top button