Wataalam chuo cha maji kusimamia miradi mikubwa

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ametaka kila panapokuwa na mradi mkubwa wa maji kuwepo na watalaam wa kutoka chuo cha maji na mhasibu ili kufanya miradi hiyo idumu na kupunguza changamoto ya ajira.

Akizungumza katika kongamano la pili la Kimataifa la Sayansi ya Maji linalofanyika Ubungo Plaza Dar es salaam, Aweso ameshangazwa kuona wataalam wanaotoka katika chuo cha maji kukosa ajira wakati,  kuna miradi mikubwa ya zaidi ya Sh bilioni 6 inakabidhiwa bila ya kuwa na wataalam.

Aweso amesema kuwa kila penye mradi mkubwa kama wa  hospitalini na shuleni kuwepo na mtaalam ambaye ataangalia ubora wa mradi husika.

Amesema baadhi ya mikoa wameanza mpango huo na umesaidia kuwapa ajira vijana zaidi ya 400 kutoka chuo cha maji huku miradi hiyo ikiendelea vizuri zaidi sababu ya kuwepo kwa watalaam hao.

Amelitaka  kongamano hilo litakalo isha Machi 10 mwaka huu kuja na  majibu ya changamoto ya mbalimbali za maji kwa njia ya teknolojia kwakuwa wizara inakitumia chuo hicho kufikiria kwa niaba ya wizara.

“Kuundwa kwa chuo cha maji, kiliundwa mahususi kwaajili ya kuzalisha wataalam ambao wataweza kuisaidia sekta ya maji na kufanya tafiti ambazo changamoto zinazoikumba wizara ya maji kije na majawabu .

Teknolojia imebadilika mazingira yamebadilika chuo cha maji lazima mufanye uchunguzi wa kuhakikisha teknolojia zilizopo sasa zinaleta mabadiliko makubwa katika wizara ya Maji” alisema Waziri Aweso.

Aliongeza pia kwa kutaka chuo cha Maji kisijifungie lazima waangalie teknolojia inavyobadilika na kuwaunganisha na wizara ili kuendana na mabadiliko ilikuendana na dhamira njema ya kumtoa mama ndoo kichwani.

Habari Zifananazo

Back to top button