Wataalam Kishapu waichambua bajeti ya Sh bilioni 12

VIONGOZI wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka kata tisa zilizojengewa uwezo na mtandao wa jinsia Tanzania TGNP kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wamepitia tathmini na kuichambua bajeti iliyotengwa zaidi ya Sh billioni 12.9 kwa mwaka 2023/2024.

Kata hizo nii Mwaweja, Mondo, Songwa, Ukenyenge, Mwadui Lohumbo, Kiloleli, Bunambiu na Kishapu na Maganzo.

Akiwasilisha uchambuzi wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia hapo jana mbele ya wataalam mbalimbali kutoka halmashauri hiyo mshauri muelekezi wa miradi kutoka Mtandao wa TGNP Joseph Abila alisema asilimia 7.3 ya pesa zilizotengwa zimepokelewa na asilimia 49 ya fedha hizo zimetumika hadi mwezi Septemba 2023.

Advertisement

Abila alisema katika bajeti hiyo kumekuwa na ongezeko la asilimia tatu kutoka bajeti ya mwaka 2022/2023 ya zaidi ya shilingi bllioni 12.6.

Abila alisema sekta ya elimu imeongoza kutengewa bajeti ya asilimia 56.08 kwa kuiboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya madarasa kwa halisi inaonyesha bajeti hiyo kuwiana na bajeti ya TGNP.

“Hakuna budi kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa juhudi za kutatua Kero za wananchi kupitia utekelezajj wa bajeti za Shughuli za maendeleo ya wilaya”alisema Abila.

Ofisa mipango wa halmashauri hiyo Joyce Mathias alisema baadhi ya miradi imeshindwa kutekelezeka kwa mwaka wa fedha huu baada ya kuangalia vipaumbele vilivyowekwa na eneo lenye idadi kubwa ya watu.

Mathias alisema mchakato wa bajeti ni jumuishi unaanzia ngazi ya vitongoji hadi taifa na halmashauri huwa wanachukua mapendekezo yote nakuyachakata Kisha kuyapeleka kunako husika na kuletewa bajeti ya kutekeleza miradi na matumizi yake

Anjela Mahona mwanakituo cha taarifa na maarifa kutoka kijiji cha Bulimba na Kulwa Jadikile kutoka kituo cha taarifa na maarifa kijiji cha Mwaweja alisema wafanye kazi ya kufuatilia miradi itawapa nafasi ya kuhoji nakujua wapi wametekeleza na wapi bado na gharama yake pia vizuri kuunda kamati ya ufuatiliaji nakutoa ripoti kwenye jamii.