Wataalam kupatiwa mafunzo huduma mishipa ya fahamu

MADAKTARI na Wataalam wa huduma za afya nchini wanatarajia kunufaika na mafunzo ya siku nne ya mishipa ya fahamu na ubongo na magonjwa mengine.

Mafunzo hayo yatakayohusisha zaidi ya nchi 15 za Jangwa la Sahara yatotolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuanzia Oktoba 28-31 mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo leo Oktoba 28, 2023 kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, mgeni rasmi kutoka Wizara ya Afya, Asha Mahita ambaye ni Mratibu Tiba Utalii, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wataalam ujuzi zaidi katika utoaji huduma za afya.

Alisema uhitaji wa mafunzo hayo ni mkubwa kwasababu wataalam wabobezi wa mishipa ya fahamu ni wachecha na hawazidi 20 nchi nzima.

“Jinsi watavyookaa kwa hizi siku nne warafundishwa lakini kwakuwa vyama viko mbalimbali watapanga mikakati jinsi gani ya kuongeza uhitaji, mafunzo tunahitaji ila ni gharama tunahitaji kuungwa mkono.” amesema Mahita.

Ametoa takwimu kuwa asilimia 30 ya watu wanapata ugonjwa wa kiharusi, na kwamba kila baada ya dakika tano kuna mtu anapata kiharusi, hivyo kuna uhitaji mkubwa kwenye kuwapa ujuzi wataalam wa afya.


Naye, Naibu Mkurugenzi Mtendaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Julieth Magandi amesema kupitia mafunzo hayo yatajenga uwezo kwa wataalam wa afya, lakini pia ushirikiano katika kubadilisha ujuzi na huduma pia.

Amesema ugongwa wa kiharusi umekuwa changamoto kubwa hivyo lazima kuwe na ushirikiano na wataalam wengine katika kumaliza shida hiyo.

“Wito wetu kwa Wananchi wawe na tabia ya kupima kabla matatizo hayo hayajatokea, tunafahamu kisababishi kikubwa cha kiharusi ni shinikizo la juu la damu.” amesema.

Akitoa ufafanuzi, Profesa wa huduma za mishipa ya fahamu kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Wiliam Matwiga amesema wataalam waliopo ni wachache hivyo uwepo wa mafunzo hayo utasaidia kuongeza ujuzi kwa waliopo.

“ Hizi kozi kwa sasa ni zamu yetu, hawa wamesoma kwahiyo tunakumbusha tu, lazima tukumbushane washughulikie mishipa ya fahamu.” amesema Prof. Katwiga.

Habari Zifananazo

Back to top button