“Wataalam wa afya kuweni na weledi”

WATAALAM wa sekta ya  afya mkoani Mtwara wametakiwa kuzingatia weledi wanapowahudumia wagonjwa kwenye maeneo yao ya kazi.

Rai hiyo imetolewa wakati wa mafunzo ya siku tatu kwa wataalamu hao kuhusu afya ya mama na mtoto yaliyofanyika wilayani Masasi mkoani humo na kukutanisha wataalam kutoka kwenye halmshauri sita kati ya tisa zilizopo mkoani humo.

Mafunzo hayo yana lengo la kupata mrejesho kutoka kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa katika vituo mbalimbali vya afya mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema manung’uniko ya baadhi ya wataalam kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa yanadhohofisha sekta hiyo na umma.

‘’Niendelee kuwasisitiza zingatieni weledi, boresheni kauli katika kutoa huduma kwa wateja, wagonjwa wetu, manung’uniko ya baadhi ya wenzetu kutoa lugha mbaya yanasikika kila siku’’amesema Abbas

Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa ikiamini kwamba msingi mkubwa ni afya zilizo imarika kwa wananchi wake, akili timamu, maarifa ya kuweza kutatua changamoto za kila siku.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Frank Omollo amesema wanataka kujua wananchi wanasemaje juu ya huduma hizo na wameona ni sehemu ya ufumbuzi kwa kuwa unawaunganisha na wananchi.

‘’Tunategemea matokeo mawili kuna wanatakao furahia huduma watapongeza ambao hawataridhishwa watatoa maoni, tutayafanyia majumuisho ili kila halmashauri iweze kutoa huduma kadri ya mahitaji na matakwa ya wananchi’’

Mkufunzi wa Kitaifa wa Mpango wa Mama na Mtoto, Rosemary Nazar amesema mpango huo umeanza kutekelezwa mwaka 2017 kwa lengo la kupunguza vifo zinavyotokana na uzazi kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga.

Hata hivyo kuboresha huduma hiyo ya mama na mtoto kwa kutoa maoni kutoka kwa akina mama hao wajawazito, waliyojifungua mpaka mtoto wa umri wa siku 28.

Habari Zifananazo

Back to top button