Wataalamu: Matokeo ya tafiti ya Saratani yaiva

DAR ES SALAAM: Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya huduma za Afya ya Aga Khan Tanzania na Aga Khan Foundation, imeandaa warsha ya kusambaza taarifa za Kitafiti za Huduma za Saratani nchini Tanzania (Data Dissemination Workshop) iliyolenga katika kutoa matokeo ya tafiti zilizofanywa na mradi huo chini ya Afua ya Tafiti za Saratani (Beat Cancer Research Initiative-BCRI).

Hayo yamejiri Desemba 12, 2023 Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa afya na kuangalia tafiti, changamoto na hali halisi ya upatikanaji na uhitaji wa huduma za saratani nchini.

Aidha,Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Mang’una amewapongeza washirika, wadau na wafadhili na watafiti vijana wa mradi huo kwa kushirikiana katika kukusanya na kuchakata taarifa hizo

Pia, Meneja wa mradi wa TCCP, Dk. Harrison Chuwa amesema matokeo ya utafiti,upatikanaji na uhitaji wa huduma za saratani utawataarifu wadau mbalimbali wa sekta ya afya na serikali kwa ujumla juu ya hali halisi ya ugonjwa na huduma za saratani. Hii itawasaidia katika kuboresha afua za upatikanaji na utoaji huduma za saratani katika vituo vya kutolea huduma za Afya na jamii kwa ujumla.

Mradi tambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) unatekelezwa katika mikoa miwili ambayo ni Dar es Salaam na Mwanza ili kupanua miundombinu iliyopo ya saratani na kutoa huduma ya kina zaidi ya saratani kupitia uimarishaji wa mifumo ya afya na kujenga uwezo kwa watumishi katika taasisi shiriki ili kutoa huduma bora ya saratani kwa wataalamu waliopata mafunzo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button