Wataalamu wa afya wapewa mbinu koboresha huduma

DAR ES SALAAM: Wataalamu na watoa huduma za afya nchini wametakiwa kujifunza zaidi njia mpya na zinazoendanda na mabadiliko ya teknolojia katika kupambana na vijidudu sugu vya magonjwa mbalimbali hali itakayosaidia kuboresha afya za wananchi.

Hayo yamebainishwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kutoka hospitali ya taifa ya muhimbili Wanin Athman ambapo ameongeza kuwa kuna umuhimu wa kuongeza utolewaji wa elimu ya afya kwa madaktari juu ya umuhimu wa kubadilisha mbinu za kutibu bakteria mbalimbali kulingana na mabadiliko ya bakteria hao.

Mkurugenzi wa kampuni Castfarm limited Anwar Kachra amesema lengo ni kutoa elimu kwa watoa huduma za afya ili kuwawezesha kukabiliana na vijidudu sugu kulingana na mabadiliko ya teknolijia huku akiishukuru serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini.

Naye Mtaalamu wa maabara kutoka hospitali ya taifa ya muhimbili James Kalabashanga amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto ya usugu wa vijidudu kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya dawa hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ufanisi wa huduma za dawa na matibabu nchini.

 

Habari Zifananazo

Back to top button