Wataalamu wapya kuongeza nguvu huduma za afya

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameziagiza halmashauri zote nchini kuajiri wataalamu wa afya wa mikataba ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma bora na haraka kwa wananchi.

Waziri Ummy ametoa agizo hilosiku ya leo Julai 13, 2023 wakati akiongea na timu ya usimamizi wa afya ya mkoa pamoja na wataalamu wa afya ngazi ya Jamii kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara yake mkoani humo.

Aidha, Waziri huyo ametaka huduma bora za uangalizi kwa watoto wachanga (NICU) ziwepo katika hospitali za halmashauri zote nchini ili kuokoe maisha ya watoto.

Advertisement

“Tunachotaka ni kuhakikisha kila mzazi anaekwenda kujifungua katika hospitali atoke na mtoto wake,” alisema waziri Ummy.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *