WATAALAMU wa afya, wameshauri walaji nyama pori kuacha, kwani baadhi ya wanyama ni chimbuko la virusi vya marburg.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Mwanza, Lenard Mlyakado, ametaja wanyama hao kuwa ni popo, tumbiri na swala.
“ Endapo kwa namna yoyote mtu atagusa mnyama mwenye virusi hivyo au kula nyama yake ataaMbukizwa haraka,” amesema Mlyakado wakati wa mkutano wa kutoa elimu ya kujikinga na marburg, uliohudhuriwa na makundi mbalimbali, ikiwemo viongozi wa dini, wafanyabiashara wadogo pamoja na wavuvi.
“Na anayepata virusi kutoka kwa wanyama ni rahisi kuambukiza binadamu wenzake pale wanapogusa majimaji yoyote kutoka mwilini mwake, ikiwemo damu, jasho ,mate au machozi,” amesema na kusistiza kwamba:
“Tahadhari ni muhimu kwa sababu hakuna chanjo wala tiba ya marburg, ispokua huduma zinatolewa kulingana na dalili alizonazo mgonjwa,” amesema.
Amesema tayari mkoa umetenga vituo maalum vua huduma na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kada zote, ikiwa ni jitihada za kujikinga na kutibu marburg, ikitokea virusi vimeingia Mwanza.