Wataalamu wataka fidia ya haraka athari mabadiliko tabianchi

BAADA ya Kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchini (COP28) Dubai, Falme za Kiarabu wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi na uchumi  wametaka kufanikishwa  kwa haraka  mfuko wa hasara na uharibu kwa nchi zinazoendelea ili kusaidia waathirika.

Wataalamu hao wametaja hatua ya utoaji wa fedha hizo kuwa ni mafanikio makubwa katika mkutano huo kwani mfuko huo ulihitajika muda mrefu.

Akizungumza na HabariLEO,Mkurugenzi wa Powershift Afrika, Mohamed Adow amesema uhitaji wa fedha za haraka ni mkubwa kwa nchi zilizoendelea hasa zile ambazo tayari madhara ya mabadiliko ya tabianchi yameshaonekana.

“Inafurahisha kuona Mfuko wa Hasara na Uharibifu unaanzishwa kwani mwanzoni mwa COP27 nchini Misri watu wengi walisema  hautakubaliwa Hiyo inaonyesha jinsi mchakato huu wa Umoja wa Mataifa unaweza kuchukua hatua za haraka kusaidia nchi zinazoendelea.

Amesema japokuwa mfuko huo umepishwa lakini hakuna sheria zinazosimamia mfuko huo kufanya kazi ambapo hakuna ulazima wa kuchangia mfuko huo licha ya kuwa mataifa tajiri  ndio yanasababisha uharibifu  huku mataifa yanayoendelea yakiwa katika hatari.

“Ni muhimu benki ya Dunia kufanya kazi hiyo kazi  lasivyo tutahitaji kuanzisha chombo tofauti kufanya kazi hiyo na suala muhimu zaidi sasa ni kupata pesa zinazoingia kwenye mfuko na kwa watu wanaohitaji,tunatarajia viongozi kuahidi fedha hapa kwenye COP28 lakini zisiwe tu ahadi,”amesisitiza.

Amesema fedha zinahitaji kama ruzuku na sio mikopo kwani mikopo itazidisha madeni kwa nchi zinazoendelea na kurudisha nyuma maendeleo yao.

Mtaalamu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Semboja Haji  ameeleza kuwa nchi zilizoendelea ndio wahusika wakubwa wa mabadiliko hayo hivyo hawana budi kufidia hasara inayopatikana kwa watu wasio na hatia.

Jumla ya ahadi zilizotolewa katika mkutano huo ni Sh trilioni 1.3 ambapo Umoja wa Falme za Kiarabua umeahidi Sh bilioni 251.5, Ujerumani Sh billion 251.5, Uingereza Sh bilioni 127.7, Marekani Sh bilioni 42.7, Japani imetoa Sh bilioni 25.15 na Umoja wa Ulaya Sh bilioni 616.3.

Habari imewezeshwa na MESHA na Ofisi ya Afrika ya IDRC Mashariki na Kusini.

Habari Zifananazo

Back to top button