Watahiniwa 613 wafaulu mitihani Bodi ya Ununuzi na Ugavi

WATAHINIWA 613 kati  ya 1,136 waliofanya mitihani ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi wamefaulu,watahiniwa 48 wamefeli na 474 watarudia mitihani

Akitangaza matokeo ya 25 ya Bodi  leo jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi  hiyo Godfred Mbanyi álisema kuwa mitihani hiyo ilifanyika Novemba 22 hadi 25  mwaka jana nchi nzima .

Álisema kuwa jumla watahiniwa 1,216 walisajiliwa ili kufanya mitihani hiyo, ambapo watahiniwa 1,135 sawa na asilimia 93.3 walifanya mitihani hiyo.

“Kumekuwepo na ongezeko la watahiniwa ukilinganisha na  msimu uliopita uliokuwa na watahiniwa 1,032” álisema

Álisema kuwa kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 452 ni wapya na waliobakia 683 ni watahiniwa waliokuwa wakirudia baadhi ya masomo.

“Jumla ya watahiniwa 613 sawa na asilimia 54 walifaulu mitihani yao,watahiniwa 474 sawa na asilimia 41.8 watarudia baadhi ya masomo kuanzia somo moja hadi masomo matatu kutegemeana na idadi ya masomo aliyofeli na watahiniwa 48 sawa na asilimia 4.2 wamefeli masomo yote waliyofanya katikae ngazi mbalimbali,” álisema.

Katika masomo  34 waliyopimwa watahiniwa, masomo 28  yalifanywa vizuri, masomo 10 yalifanywa kwa wastani na matokeo ya masomo sita yalikuwa mabaya kwa maana ya kuwa chini ya wastani. Aidha watahiniwa watatu wialiibuka Kama watahiniwa bora.

Habari Zifananazo

Back to top button