Watakiwa kubomoa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara

KAGERA: Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa amewataka wananchi wote waliojenga ndani ya hifadhi za barabara katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kuanza kujiandaa kisaikolojia na kuondoka wenyewe kabla ya serikali kuanza kubomoa ili kupanua ujenzi wa barabara.

Bashungwa aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua upanuzi wa barabara ya Rwamishenye _ kastamu maarufu kama Uganda road inayojengwa Kwa njia nne katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa gharama ya Sh bilioni 4.6.

Advertisement

Alisema kuwa ili mradi usikwame na mkandarasi kuanza kazi kwa wakati wananchi wanapaswa kupisha ujenzi na kuzingatia sheria za barabarani huku akipongeza wananchi ambao wamebomoa wenyewe na kusema kuwa ili kupunguza ajali za mara kwa mara ni lazima mradi huo utekelezwe kwa wakati na kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa wa KAGERA Mhandisi Ntuli Mwaikokesya alisema mradi huo unatekelezwa na mkandarasi mzawa ikiwa ni awamu ya kwanza lakini awamu ya pili itakuwa ni kutoka Mitaga Hadi stendi eneo la TRA mita 600 lakini Kwa hii awamu ya kwanza itatekelezwa Kwa muda wa miezi kumi na mbili.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *