Watakiwa kuchangamkia fursa mikopo boti za uvuvi

WAZIRI wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amewataka wananchi hasa vikundi vya vijana na wanawake wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi na kilimo cha mwani kuchangamkia fursa ya kuomba mkopo wa boti zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza leo mkoani Mtwara alipokagua mradi wa kituo cha ukuzaji viumbe vya majini uliyopo kijiji cha Ruvula kata msimbati mkoani humo Waziri huyo amesema mwisho wa maombi hayo ni Januari mwishoni 2024.

Tukio hilo limefanyika leo Januari 14, 2024 katika kijiji cha Ruvula kata ya Msimbati Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani humo.

Aidha mradi huo utahusisha uzalishaji wa viumbe mbalimbali wa majini ikiwemo samaki, jongoo bahari, kaa lakini pia kilimo cha mwani na vingine uliyogharimu zaidi ya Sh milioni 800.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema mradi huo umekuja muda mwafaka katika maeneo hayo kutokana na historia ya eneo la msimbati huko nyuma wanajishughulisha na shughuli za jongoo pamoja na uvuvi.

“Uwepo wa soko la mazao ya bahari umezidi kuongezeka kutokana na kuwa karibu na nchi jirani ya comoro ambayo inauhitaji mkubwa wa chakula cha mifugo na mazao ya bahari”amesema Abbas.

Hata hivyo uwepo wa kituo hicho kunaenda kuongeza kasi ya biashara baina ya nchi hizo mbili jambo litakalowezesha kuongezeka kipato kwa wananchi hao na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa wavuvi katika kata hiyo, Ally Mzaidi ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili wanapotekeleza majukumu ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kuvulia vya kisasa hivyo kushindwa kufanyakazi kwa ufanisi.

“Sisi wavuvi wa msimbati tuna changamoto ya vifaa tunatumia mitumbwi ya kizamani ya kusukuma na miti kwahiyo tunaiomba serikali kutusaidia kupata vifaa vya kisasa”amesema Mzaidi

Habari Zifananazo

Back to top button