Watakiwa kudhibiti waharibifu vyanzo vya maji

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukuwa hatua kali dhidi ya watu wanaochepusha maji bila vibali na wanaoharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughuli za uchimbaji wa madini usio rasmi.

Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya kutembelea vyanzo vya maji  na mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Tanga na Muheza.

“Iwe ni marufuku kwa wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji kuharibu vyanzo hivyo kwa shughuli za kibinadamu pamoja na kuchepusha maji bila vibali maalumu,”amesema RC Kindamba.

Amezitaka taasisi za umma ambazo zina madeni makubwa ya ankara za maji kulipa madeni yao, ili kusaidia shughuli za uendeshaji kwa Tanga Uwasa.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa, Mhandisi Geoffrey Hills amesema kuwa mradi wa upanuzi wa huduma ya maji utasaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita Mil 30 hadi Mil 45.

“Tunaomba serikali itusaidie kuhakikisha baadhi ya taasisi zake zinatulipa malimbikizo ya madeni yao, ambayo yamefikia takribani Sh Bil 9.6,”amesema Mhandisi Hills

Habari Zifananazo

Back to top button