Watakiwa kuendeleza vijana wabunifu wa kisayansi

SHIRIKISHO la Wanasayansi Chipukizi Tanzania (YST) limetoa wito kwa wadau ikiwemo sekta binafsi kujitokeza kuendeleza vijana ambao wamebuni kazi za kisayansi zinazolenga kutatua na kukabiliana na matatizo yanajitokeza kwenye jamii nchini.

Mwanzilishi mwenza wa shirikisho hilo, Dk Gozibert Kamugisha ametoa wito huo huku akisema kuna idadi kubwa ya kazi nzuri ambazo zimebuniwa na vijana kutoka shule za sekondari nchini lakini bado hazijaendelezwa kwa manufaa ya nchi.

“Kuna hitajika nguvu za zaida kutoka kwa wadau wote, kwa serikali, sekta binafsi kuweza kusaidia vijana wabunifu kwenye sayansi ili zile kazi wanazozifanya ziweze kufika mbele ili kesho na keshokutwa zile kazi ziweze kusaidia nchi yetu isonge mbele,” amesema.

Advertisement

Kamugisha ametoa wito huo wakati wa maonyesho ya pili ya Kazi za Sayansi na Teknolojia Mkoa Lindi ambazo zimetengenezwa na wanafunzi kutoka shule za sekondari mkoa humu.

Maonyesho hayo yameshirikisha wanafunzi kutoka shule 15 ambapo wanafunzi Wawili wamechaguluwa kushiriki maonyesho ya kitaifa ambayo yatafanyika mwezi Disemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

6 comments

Comments are closed.