Watakiwa kujifunza mfumo mpya teknolojia

WADAU wa mahakama na wananchi kwa ujumla wametakiwa kujifunza na kushiriki majaribio ya mfumo mpya wa teknolojia ambao utatumika kuanzia Novemba Mosi mwaka huu.
Mfumo huo ni sehemu ya kurahisisha kutoa huduma na kuwawezesha watanzania kutoka kwenye makaratasi Hadi Digtal katika sehemu ya mahakama unaojulikana Kama (E-CMS)E_Kessy Management System .
Akizungumza na wadau wa mahakama mkoani Kagera Jaji Mkuu na Mwenyekiti wa Tume ya Mahakama, Profesa Ibrahim Khamis Juma alisema kuwa mfumo wa Tehama unaotumika sasa hivi kama sehemu ya tekinolojia ujulikanao (GSS2 )umezidiwa lakini tayari mfumo mpya umeanza kufanyiwa majaribio.
Amesema ni muhimu kila mdau wa mahakama anapaswa kushiriki na kuendana na mabadiliko ya sasa ya karne ya 21 ambapo karatasi mahakamani hauzitatumika tena.
Alisema kuwa Tume ya Mahakama inaendelea na ziara katika mikoa mbalimbali na kukutana na tume za maadili za mkoa, wilaya ambapo amepongeza Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kuwa mashauri yote ya mahakamani hapo kwa asilimia 99 wanatumia digitali na tayari wameshahama katika matumizi ya analojia.
Aidha ametuma ombi la serikali kuhakikisha kasi ya umeme unaosambazwa vijijini usiache myuma mahakama za mwanzo kwani matumizi ya teknolojia yanahitaji umeme hivyo watumishi wote na wananchi watalazimika kutumia huo mfumo ambapo mahakama zote zitapaswa kuwa na huduma ya umeme.
Mfumo huo mpya unatarajia kutumika kufanya usajili wa mashauri mahakamani ,kutunza kumbukunbu za kesi ,kutoa hukumu,kukata rufaa na huduma zote za haki ikiwemo kurahisisha muda na kupunguza mashauri haraka mahakamani ambapo Mwananchi atafatilia mwenendo wa kesi yake na kupata taarifa hata kupitia simu janja.
“Tunaendelea kukumbushia maadili ya watumishi wetu wa mahakama,uwezi kutoa haki kama hauna maadili mazuri ,mifumo mipya ya teknolojia itarahisisha haki za Wananchi na utoaji huduma ambapo kama mtu hatoridhika atatoa malalamiko yake na tutapata kupitia mfumo,watumishi wetu wanapaswa kuwa weledi na wenye mifano ya kuigwa katika jamii,kutoa haki bila upendeleo,kujali muda ,kufanya kazi kwa wakati na haraka na kuhakikisha wananchi wanapata huduma sitahiki.”Alisema Juma.
Akizungumzia matarajio ya Tume ya Mahakama na wadau wa mahakama kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Jaji Kiongozi Mustapher Siyani alisema kuwa serikali inaendelea kusogeza huduma kwa wananchi na matarajio ya tume hiyo ni kuwa kila Tarafa Tanzania kuwa na mahakama moja.
Alisema Tanzania inamahakama 947 Kati ha hizo mahakama 147 hazitumiki kutokana na uchakavu wa majengo na miundombinu, mahakama 212 zinatembelewa na mahakimu hazina watumishi wa kutosha ,mahakama 29 maeneo yake yamevamiwa na wanachi wanaoendelea kufanya shughuli nyingine.
Alisema hili kusogeza huduma kwa wananchi kwa mwaka 2023/2024 mahakama 60 zitajengwa na serikali Kama sehemu ya kusogeza huduma kwa wananchi huku akitoa wito kwa wenyeviti wa mitaana vijiji kulinda maeneo ya mahakama yasivamiwe na wananchi kwani Serikali inampango wa kuyaendeleza na kusaidia wananchi wake kupata haki kwa haraka na kuwapunguzia mwendo mrefu .