Watakiwa kushiriki mapambano ukatili wa kijinsia

KAMATI  za shule za msingi zimetakiwa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Usevya Development Society (UDESO), Eden Wayimba, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili kwa Kamati za Shule za Msingi Lugonesi na Kasekese zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina hiyo ofisa elimu awali na msingi Wilaya ya Tanganyika,. Gidion Bunto amezitaka kamati hizo kutimiza wajibu wao kwa kufuatilia mienendo ya wanafunzi kitabia, kitaaluma ikiwemo kusimamia ulinzi wa miundombinu ya shule.

Advertisement

Ametoa wito kwa kamati hizo kutoa ushirikiano kwa walimu pale inaporipotiwa mwanafunzi kabebeshwa ujauzito na si kuwaachia walimu washughulikie suala hilo pekee.

Semina hiyo imefadhiliwa na UDESO kwa kushirikiana na taasisi ya WAJIBU inatarajia kutekeleza mradi wa uwajibikaji katika sekta ya elimu msingi (AAI) katika Vijiji vya Kasekese na Lugonesi.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *