Watakiwa kushirikisha jamii zote bila ubaguzi

Watakiwa kushirikisha jamii zote bila ubaguzi

WAUMINI wa dini ya kiislaam mkoani Katavi, wametakiwa kushirikisha jamii zote bila kubagua dini wala kabila pale wanapokua na jambo linalohitaji mkusanyiko wa watu, ili kuendelea kudumisha upendo na amani kwa dini zote nchini.

Hayo yamesemwa na Shekh wa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu katika futari iliyoandaliwa na mmoja wa waumini wa dini hiyo Mhandisi, Ismail Nassoro.

Amesema kwa kufanya hivyo ni kuendeleza umoja ulioanzishwa na muasisi wa Taifa la Tanzania, hayati Mwalimu Julius Nyerere kushirikiana bila kujali itikadi za dini, vyama, rangi na kabila.

Advertisement

“Tunamskuru sana bwana Ismail kutuchanganya jamii zote, imezoeleka kufanya hivi ni kwa taasisi tu, ila yeye kafanya kama mtu binafsi, hivyo atakua amefungua mlango hata kwa watu wengine wanapoandaa futari au tukio linalokutanisha watu basi wasichukue upande mmoja,” amesema Shekh Kakulukulu.

Naye muandaaji wa futari hiyo, Mhandisi Ismail amesema ameguswa kufanya hivyo kutokana na maelekezo ya dini ya kiislaam kuwa ukifuturisha unapata thawabu, huku akisema katika jamii ya watu wa Mpanda kuna wenye uhitaji na wasiokua na uhitaji, hivyo katika kujenga umoja na mshikamano ameamua kuwakutanisha pamoja dini zote, taasisi, viongozi wa vyama vya siasa, serikali na wengine.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa futari hiyo wametoa shukrani kwa muandaaji kwa jambo kubwa alilofanya bila kujali itikadi wala kubagua mtu wa aina yeyote.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *