KATIKA kuboresha huduma za afy, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk Seif Shekalaghe ametoa wito kwa makatibu wa afya nchi nzima kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Makatibu wa Afya Tanzania (AHSTA) leo Mei 17.2023 Jijini Mwanza Dk Shekalaghe amesema kuwa ni vyema kwa watoaji wa huduma za afya kutumia lugha nzuri kabla na baada ya kumuhudumia mgonjwa.
Katika hatua nyingine Dk Shekalaghe ametumia fursa hiyo kuwahaidi Makatibu hao wa afya kushughulikia jambo la uanzishwaji wa baraza la kitaaluma kwani itasaidia kuboresha muundo mzima wa kada hiyo huku akihaidi kuzungumza na Katibu Mkuu Tamisemi ili kulipatia ufumbuzi mara moja jambo hilo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Juliana Mawala amesema kuwa jambo la kutokua na baraza inasababisha kukwamisha usimamizi wa masuala ya kinidhamu kwa watumishi wa kada hiyo ya Afya na muundo mpya kutomtambua katibu wa Afya kama msimamizi mkuu.
Kwa upande wao makatibu wa afya, Lilian Musin na Frank Omolo wamesema kuwa maelekezo waliyopewa watayafanyia kazi kutokana na Serikali ya hawamu ya Sita kuwekeza miundombinu ya kisasa katika katika sekta ya afya.
Mkutano mkuu huo wa mwaka wa makatibu wa makatibu wa afya Tanzania (AHSTA) unafanyika kwa siku tatu huku kauli mbiu ikisema kuwa uwekezaji na uhimalishaji wa mifumo ya afya Nchini ni msingi wa utoaji huduma bora kwa wananchi.