Watakiwa kutopandisha bei

MWENYEKITI  wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman amewasihi wafanyabiashara katika masoko  kutopandisha bidhaa kiholela hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Rai hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kutembelea masoko ya mgandini na Ngamiani kujionea hali ya utoaji wa huduma na kusikiliza kero zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Amesema, kumekuwa na changamoto ya upandaji wa bidhaa hasa zile ambazo zinatumika sana na waumini wanaofunga  hususani kipindi hiki cha mfungo hali ambayo inawapa shida watumiaji wa bidhaa hizo.

“Kama mnavyojua kufunga ni ibada hivyo rai yangu wafanyabiashara licha ya changamoto ya ukame lakini niwaombe muwe na utu katika swala la Bei wekeni bei ambazo kila mtu atamudu kununua”amesema Mwenyekiti huyo.

Nae afisa biashara wa Halimashauri ya Jiji la Tanga Rose Marandu amesema kuwa upandaji wa bidhaa umeathiriwa na ukame kwani bidhaa zinazotoka mashambani no chache tofauti na hapo awali.

“Toka mwezi Januari mwaka huu kumekuwa na changamoto ya uhaba wa mazao hivyo bei imekuwa ni changamoto lakini tunaendelea na jitihada za kuongea na wafanyabiashara kuweza kuuza kwa Bei ya faida kidogo  ili  kutomuumiza mwananchi wa kawaida.

Habari Zifananazo

Back to top button