Watakiwa kutumia elimu ya kilimo kujikwamua kiuchumi

MOROGORO: Ofisa tawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya kilombero Wakili Innocent Magesa amewataka wakazi wa Man’gula na vitongoji vyake kutumia elimu na maelekezo ya utunzaji wa mazingira iliyotolewa na wataalamu mbalimbali katika uzinduzi wa msimu wa kilimo Wilaya ya Kilombero.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mashada vilivyopo Man’gula na kuwakutanisha wadau mbalimbali Katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Kauli mbiu katika uzinduzi huo ni”Jitambue Badilika acha Mazoea Timiza Wajibu”, mbali na uzinduzi huo palikuwa na maonyesho ya zana za kilimo, mifugo, madawa, na mazao mbalimbali.

Ofisa huyo amesema ni vizuri kuzingatia maelekezo na ushauri wa kitaalamu katika matumizi ya viuatilifu, na mbolea na kuifadhi sehemu sahii makopo, na vifungashio ili kutunza mazingira na kuepukana na madhara kama magonjwa ya kansa.

Kwa upande wake mlezi wa Taasisi ya Mazingira ni Uhai Foundation Abdon Mapunda amesema malengo ya taasisi hiyo ni kutunza mazingira ya mji wa ifakara, kuhakikisha kipato kinaongezeka kwa wanachama ambao wengi wao ni wakulima.

Hata hivyo mpaka sasa wanachama wanakadiriwa kufikia 200, na mlezi ameaidi kuwapatia bima ya afya kufikia julai 2024, pia amewataka wakulima kulima kilimo chenye tija na kujikwamua kiuchumi.

Habari Zifananazo

Back to top button