Watakiwa kutumia mikopo kwa malengo

MKUU mpya wa Wilaya ya Chato mkoani Geita, Deusdedith Katwale amewataka wajasiriamali ambao ni wanufaika na mikopo ya halmashauri kuzingatia maandiko mradi waliyowasilisha, ili mikopo wanayopata iwe na tija.

Katwale ametoa maelekezo hayo Januari 31, 2022 wakati akikabidhi mkopo wenye thamani ya Sh milioni 178 kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Amesema ili kufikia malengo yao ni lazima wanachama wa vikundi kuwa waadilifu na kufanya kazi kulingana na andiko mradi na kuacha kutumia mkopo huo kila mmoja kwa malengo yake.

Katwale amewatahadharisha, wanaposhindwa kuyaishi maandiko mradi huenda ikasababisa vikundi vyao kutojiendesha kwa faida na hatimaye kutomudu kufanya marejesho ya mikopo hiyo.

“Ndugu zangu wananchi wa Chato, serikali yenu inawapenda na mheshimiwa Rais ana imani kubwa  nanyi, hivyo onesheni fadhila kwa  kufanya kazi, ili sote kwa pamoja tujiletee maendeleo,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button