Watakiwa kuwapa mikataba ya ajira watumishi

WAAJIRI nchini wametakiwa kutoa mikataba ya ajira sambamba na stahiki nyingine kwa watumishi wao kama ambavyo, sheria za kazi zinavyoelekeza.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya ya Tanga, Hashim Mgandilwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba, wakati wa sherehe za wafanyakazi Uwanja wa  Mkwakwani jijini Tanga.

Amesema kuwa bado kuna changamoto ya waajiri wengi hususani katika sekta binafsi, kutotimiza wajibu wao kwa kutotoa mikataba ya ajira pamoja na stahiki nyingine kwa watumishi wao, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

“Niwaagize ofisi ya kazi kuhakikisha mnatembelea waajiri wote, ili kujiridhisha kama wanafuata masharti ya utoaji wa mikataba kwa watumishi wao na kama hawafuati kuwachukulia hatua stahiki, “amesema DC Mgandilwa.

Naye Mratibu wa Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Tanga, Athuman Kayumba ameiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kazi, ili watumishi waweze kufanya kazi zao vizuri.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x