Watakiwa kuzingatia kanuni za afya

Watakiwa kuzingatia kanuni za afya

WANANCHI wilayani Tanganyika mkoani Katavi wamehimizwa kuzingatia kanuni za afya, ikiwa ni pamoja na kuwa na utamaduni wa kujenga vyoo bora, ili kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu alipozungumza na wananchi wa Kata ya Karema katika ziara yake kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ofisa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Henrick Mwasibale, amewaeleza wananchi wa Karema kuwa iwapo watazingatia ujenzi na matumizi ya vyoo bora pamoja na kuchemsha maji kwa usahihi au kutumia vidonge vya kusafishia maji, pamoja na kujenga utamaduni wa kunawa mikono mara kwa mara, itasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu.

Advertisement

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu akipozungumza na wananchi wa Kata ya Karema.(Picha zote na Swaum Katambo).

Kwa upande wao wananchi wa Karema wameiomba serikali kushughulikia kwa karibu changamoto ya uhaba wa maji, hasa katika kituo cha afya Karema kwa kuwa kutopatikana kwa huduma ya maji ya uhakika kituoni hapo kunahatarisha usalama wa afya za wagonjwa na wakazi wa eneo hilo.

Kutokana na changamoto hiyo, Meneja Ruwasa Wilaya ya Tanganyika, Mhandisi Alkam Omary, amewatoa hofu wananchi wa Kata ya Karema na kueleza kuwa changamoto ya uhaba wa maji kituoni hapo, ilipatiwa ufumbuzi kwa kurekebisha pampu kutokana na  kuungua kwa pampu ya maji.

Amesema hadi sasa taratibu za ununuzi wa pampu nyingine unafanyika hatua itakayoondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa maji katika eneo hilo kwa kuwa kutakuwa na pampu mbili.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *